• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wadau Wakutana Kutathimini Utekelezaji wa Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira

Posted on: February 14th, 2019

Viongozi na wawakilishi wa wananchi kwa ngazi za Halmashauri, kata na vijiji wakiwemo waheshimiwa madiwani wameshauriwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao na mashirika mbalimbali inafanyika kama ilivyokusudiwa walipokuwa kwenye kikao cha wadau juu ya maendeleo ya mradi wa majisafi na usafi wa mazingira uliyopo kwenye Halmashauri za Wilaya ya Geita na Nyang’hwale.

Hayo yameelezwa na Eng. Immaculata Raphael aliyefungua kikao hicho, wakati akisoma hotuba kwaniaba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwakumbusha washiriki wa kikao hicho kuwa wanapaswa kutambua mradi huo unaelekea ukingoni, hivyo ni vyema kutumia vizuri muda na nafasi iliyopatikana katika utekelezaji wa mradi huo, huku akiwapongeza madiwani waliohudhuria kikao hicho kwa wingi na kuwashukuru watekelezaji wa mradi huo unaoshirikiana na serikali.

Amesema “nawashukuru sana waheshimiwa madiwani kwa kuhudhuria kwa wingi katika kikao hiki muhimu, vile vile niwashukuru wadau mnaoshiriki kutekeleza mradi huu. Niwaombe viongozi tutambue yakuwa muda si rafiki na unakaribia kuisha kwakuwa mradi ni wa miaka minne tangu mwaka 2016, hivyo tujipange kuendeleza pale wadau watakapoachia kwakuwa ni dhahiri kuwa hata wengine nao wanahitaji msaada wao”.

Eng. Raphael amewakumbusha wajumbe hao juu ya umuhimu wa kutambua kwamba lengo la mradi ni kupunguza vifo vya kina mama na watoto vitokanavyo na uzazi kwa kuboresha miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya na kuboresha upatikanaji wa majisafi na salama bila kusahau kuinua kiwango cha usafi wa mazingira ngazi ya kituo cha afya, shule na kaya zinazozunguka kituo, kisha kuweka kikao wazi akiamini kikao hicho kitatoa mapendekezo ya namna bora zaidi ya kuboresha utekelezaji wa mradi huu na hatimaye kupunguza vifo visivyo vya lazima.

Akiongea kabla ya hotuba ya ufunguzi, Dkt. Greyson Mbaruku ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la WEDECO amewaeleza wajumbe hao kuwa, ni vyema wakawa huru kuchangia mawazo yao katika kuboresha utendaji wa mradi huo.

Nao waheshimiwa madiwani kama viongozi wa kisiasa na wenye nafasi kubwa ya ushawishi kwenye jamii wakiongozwa na wenyeviti wa Halmashauri hizo, wameshukuru kwa uwepo wa mradi huo na kupongeza juhudi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau, wakiahidi kuhakikisha kwenye halmshauri wanazozisimamia wanatenga fedha ili kuendeleza juhudi hizo zilizoanzishwa, kisha kuomba wadau hao wendelee kutoa ushirikiano na hata pengine kuleta miradi mingine Geita.

Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unafadhiliwa na nchi ya Canada na kutekelezwa na mashirika ya Amref Health Africa na WaterAid Tanzania, ambapo Amref wanahusika na mafunzo ya wauguzi, ujenzi wa majengo na utoaji vifaa tiba na lishe wakati WaterAid hushirikiana na wadau wa maendeleo WEDECO Ltd katika upatikanaji wa maji safi na salama, bila kusahau mafunzo ya usafi wa mazingira na tendanishi (usafi binafsi).



Matangazo

  • MATOEKEO YA KIDATO CHA SITA YATANGAZWA July 05, 2022
  • HOTUBA YA BAJETI YA NCHI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 June 01, 2022
  • BAJETI YA MKOA June 28, 2022
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Staki Senyamule Tarehe 19 Mei 2021 May 19, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • “Watumishi Jipangeni Kuwahudumia Wananchi, Ofisi Tunayo”- Asema RC Shigela

    August 06, 2022
  • “Sensa ni Kipaumbele Chetu Hadi Agosti 23, 2022”. Asema RC Shigella.

    August 05, 2022
  • “Sensa ni Kipaumbele Chetu Hadi Agosti 23, 2022”. Asema RC Shigella.

    August 05, 2022
  • Sensa si Mzaha, ni Maisha ya Watu, Tujiandae Kuhesabiwa-Asema RC Senyamule

    July 28, 2022
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa