Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita Dkt.Elfas Msenya amesema Taasisi ya Tanzania sicklecell warriors (TASIWA) kupitia mradi wake wa KETAN utaboresha maisha ya Watu wanaoishi na ugonjwa wa Selimundu( Sicklecell Anaemia) katika Halmashauri zote za Mkoa wa Geita.
Dkt. Msenya ameyasema hayo Desemba 03,2025 wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mradi wa KETAN Uliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Watenge Bajeti kwa wale wote Watakaobainika wanaugonjwa huo wapewe Bima za Afya Ili ziwasaidie kwenye matibabu Yao.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita ametoa ushauri kwa Taasisi ya TASIWA kutenga bajeti ya kuwahudumia watu watakaobainika kuwa na ugonjwa huo na kuwawezesha kupata kadi za Bima ya afya wagonjwa wote na sio kuwapa baadhi ya wagonjwa wachache.
Dkt. Msenya ameieleza Taasisi hiyo kuwa ratiba zao za kutoa elimu kwa jamii zitakapoanza wawaelimishe wananchi watambue kuwa Ugonjwa huo sio laana wala hauambukizwi,sio ushirikina na hautokani na mzazi mmoja bali ni ugonjwa wa kurithi.
Kaimu Katibu Tawala ametoa wito kwa TASIWA kuziwezesha familia zilizoathiriwa na sikoseli kupatiwa msaada wa bima za afya,Uchumi na kijamii pamoja na kupatiwa ushauri nasaha Ili kuweza kuishi na watu wenye ugonjwa huo bila kuwanyanyapaa. Pia ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Geita kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ili baada ya miaka miwili mkataba wa wahisani utakapomalizika baada ya miaka miwili mradi huo usisimame.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TASIWA Pascazia Mazenze ameeleza lengo la kuuleta mradi huo mkoani Geita limetokana na kutokuwepo kwa taarifa ya wagonjwa wa sikoseli,mradi huu utaibua wagonjwa,utatoa bima za afya kwa wagonjwa 300, na kutoa elimu kwa Jamii ya Geita kwa Kutumia redio na televisheni Ili kuondoa dhana potofu kwa Jamii dhidi ya wagonjwa wa sikoseli.
Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto na Mtaalamu wa Sikoseli Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Dkt. Emmanuela Ambrose amesema kuwa ana imani Wizara ya Afya itausimamia Vizuri mradi kama inavyosimamia miradi mingine na utaleta matokeo chanya yenye kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa sikoseli katika Jamii.
Kwa upande wake msimamizi wa huduma za maabara kutoka ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Idrissa Hassan amesema Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wana jukumu la kuwezesha utekelezaji wa sera na kuwezesha mafanikio ya TASIWA Ili huduma hizi ziwe endelevu na kuleta matokeo chanya katika Jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Waganga wakuu wa Halmashauri zote za Mkoa wa Geita ,Mganga Mkuu wa Manispaa ya Geita Dkt.Sunday Mwakyusa amesema maelezo yaliyotolewa na wizara ya Afya yatatekelezwa na kuhakikisha Mkoa wa Geita unatoa taarifa sahihi pia Halmashauri zitatenga bajeti kwa kushirikiana na wadau wa afya Ili mradi huu uwe endelevu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa