• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

“Tunaiomba Radhi Serikali”- Wananchi wa Muganza-Chato Wasema na Waziri Masauni

Posted on: April 7th, 2023

Na Boazi Mazigo - Geita

Wananchi na wakazi wa Kata ya Muganza Wilaya ya Chato Mkoani Geita wameiangukia serikali na kuiomba radhi kufuatia tukio la kubomoa na kukichoma moto kituo cha polisi Muganza, tukio walilolitekeleza  Machi 30, 2023 kwa madai ya kutoridhishwa na sababu za kifo cha mtuhumiwa wa wizi wa betri Enos Misalaba (32) ambaye kwa sasa ni marehemu ambaye ilielezwa alifariki kutokana na kuumwa lakini wao wakidai alifariki kutokana na kupigwa na askari polisi.

Hayo yamejili Aprili 7, 2023 wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mhandisi Hamad Masauni katika kata ya Muganza-Chato ambaye alieleza kusikitishwa kwake kwa kitendo kilichofanyanyika na kutoa onyo kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi akiwasihi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kudumisha amani na usalama kwa kuzingatia uwekezaji mkubwa uliopo na unaoendelea.

“kwakuwa serikali inayoongozwa na Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan inafanya kazi kubwa sana kwa maendeleo ya watu ninyi ni mashahidi, imani yangu kuwa nyie ndio kuisaidia serikali  katika kuhakikisha mnaimarisha ulinzi katika maeneo yenu, lakini msipotoa ushirikiano kwa jeshi la polisi mnaweka rehani usalama wenu. Ilinishangaza sana watu ambao hawalali kuhakikisha mnaishi salama, nyie mnakua mstari wa mbele kuhujumu rasilimali za jeshi la polisi, hili halikubaliki hata kidogo na sitarajii kuona tena suala hili baada ya ninyi kuomba radhi”, alisema Mhe.Masauni.

Mhe.Masauni aliongeza kuwa, wapo viongozi wanaowakingia kifua wahalifu kwa misingi ya kuwa ni wanachama wao, hivyo kusema inapotokea uhalifu, sheria huchukua mkondo wake kwa yeyote atakayefanya mambo kinyume na utaratibu na kusisitiza kuwa kauli kama hizo huvuruga umoja na mshikamano ambao umejengwa na Mhe.Rais Dkt.Samia.

Alimaliza kwa kuipongeza CCM kutoa jengo lake na kulifanya kituo kwa muda, kisha kupongeza juhudi za mkoa na wilaya kwa jitihada wanazozifanya kuimarisha ulinzi na kuwataka walioanza kuchangia ujenzi waendelee na wito kutolewa kwa jeshi la polisi na wote wanasimamia usalama wa wananchi kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya sheria na ikiwa kuna askari anaenenda kinyume basi ashughulikiwe na ngazi ya wilaya na mkoa

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Geita Mhe.Martine Shigela aliwakumbusha wananchi kufuata hatua mbalimbali kwa kuwaona vingozi na kuwasilisha kero zao katika kutatua changamoto kuliko kujichukulia sheria mkononi

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa Geita ACP Safia Jongo alisema yeye havumilii vitendo ambavyo si vya kiuadilifu na kuwasihi kufuata taratibu na kwamba kitendo kilichofanyika siyo cha kiutu wala si cha kibinadamu. Hivyo kuchukua nafasi hiyo kukemea na kuwataka wananchi kuheshimu dola na kuwaahidi haki kutendeka kwa waliohusika.

Awali wananchi hao walipewa nafasi ya kuongea ambapo waliwakilishwa na Bw.Dismas Joshua na Bi.Mary Josephat ambao waliomba radhi kwa serikali kufuatia tukio hilo na kuahidi kutojirudia wakisisitiza kuwa kata yao ni kubwa na ina biashara nyingi hivyo upo umuhimu mkubwa kuwa na kitio cha polisi.

Geita Bila Sheria Mkononi Inawezekana



Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Waziri Mavunde Aaagiza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nyuma Ya CSR Geita

    April 15, 2025
  • Mabonanza ya Watumishi Yawe Endelevu - DC Kingalame

    March 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa