Na Boazi Mazigo-Geita
Wajumbe wa Baraza la ardhi la nyumba Wilaya ya Geita wametakiwa kuhakikisha wanazingatia sheria, taratibu na kanuni katika kutenda haki wakati wa utatuzi wa migogoro ya ardhi huku wakisisitizwa kuwasaidia wanawake na wajane ambao wengi wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kukosa haki ya kumiliki ardhi hususan wakati wanapoondokewa na wenzi au waume zao.
Hayo yameelezwa Machi 13, 2023 na mkuu wa mkoa Geita Mhe.Martine Shigela wakati akiwaapisha wajumbe hao ofisini kwake na kumshukuru waziri mwenye dhamana na ardhi kwa kuona umuhimu na haja ya kuimarisha sekta hiyo
Mhe.Shigela ameanza kwa kumshukuru Waziri mwenye dhamana Mhe.Dkt.Angeline Mabula (Mb) kwa kuona haja ya kuimarisha baraza la ardhi na nyumba katika Wilaya ya Geita akisema, “tunataka Mkoa wetu uondokane na migogoro ya mali, ardhi ikiwemo”
“mkoa wetu una shughuli nyingi za kiuchumi, watu huongezeka lakini ardhi ni ileile, hivyo migogoro inaweza kuibuka mara kwa mara. Dhamana mliyopewa ni kubwa, hivyo nendeni mkamsaidie mwenyekiti na wananchi wa Geita kuhakikisha mnatenda haki, nitawapa ushirikiano na ofisi yangu ipo wazi”, alimaliza Mhe.Shigela
Kwa upande wake Mwenyekiti Baraza la Ardhi na Nyumba (w) Geita Bw.Edward Masao, alisema “awali tulikuwa na migogoro 450 lakini kwa sasa imebakia 195, elimu (darasa la asubuhi), mazungumzo, ndiyo chanzo cha mafanikio hivyo naamini kwa kuteuliwa wajumbe hawa ambao ni muhimu katika kunisaidia kufanya maamuzi tutaendelea kuipunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi”.
Naye Bi.Mary Masao miongoni mwa wajumbe watatu walioapishwa alisisitiza kuwa watazingatia kwa Uimara (STK) Sheria, Taratibu na kanuni katika kumshauri mwenyekiti juu ya utatuzi migogoro mbalimbali ikiwemo ile ya kudhurumiwa ardhi kwa wanawake na wajane
wajumbe hawa wameteuliwa kwa miaka 3 na Waziri wa Ardhi kwa mujibu wa kifungu cha 26(1) cha Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi na.2 ya mwaka 2002 na wameapishwa na Mkuu wa Mkoa kwa mujibu wa kanuni na.36 ya Gn.na.174 ya mwaka 2003.
Geita Bila Migogoro ya Ardhi, Inawezekana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa