• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TASAF III Yaendelea Kuwanufaisha Walengwa Nyambaya-Geita DC, Watuma Salamu kwa Serikali

Posted on: June 24th, 2019

Ni Juni 24, 2019 ambapo jumla ya kaya Sabini na Nne (74) za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF III) kutoka kijiji cha Nyambaya, Kata ya Katoma, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Wilaya na Mkoa wa Geita wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na namna wanavyoendelea kunufaika na mpango huo, huku wakitoa shuhuda za mafanikio waliyoyapata kutokana na kutumia fedha wanazozipata ipasavyo.

Pongezi hizo zimetolewa kwa serikali kupitia  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alipowatembelea walengwa hao katika ziara yake ya kikazi, ambapo amewapongeza kwa namna walivyoanzisha miradi mbalimbali ili kujikwamua na umasikini lakini pia kwa kujiunga na bima ya afya, huku akiwaahidi kufikisha salamu na shukrani hizo za pongezi kwa Mhe. Rais.

“niwapongeze viongozi kuanzia ngazi ya kijiji hadi halmashauri kwa usimamizi mzuri, nimshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuendelea kuwajali wananchi. Niwaombe wafugaji na wakulima muendelee msikate tama, wataalam watakuja kuwapa mafunzo zaidi mpige hatua, lakini vile vile niwapongeze kwa kuwa na hisa kwa kuweka na kukopa, huu ni mwendelezo mzuri ni vyema msichoke na msitumie fedha hizi kulewa na kuoa oa”, alisema Mhandisi Gabriel.


Mhandisi Gabriel ametembelea baadhi ya kaya ikiwemo ya Bi. Lucia Matome na mumewe Mzee Laurent Manyanya wa umri wa Miaka sabini na nne (74) kushuhudia ni kwa jinsi gani walengwa hao wameweza kubadilisha maisha yao kwa fedha wanazozipata na kuwatia moyo kuwa wasiogope kuchekwa, bali waendelee kuchapa kazi baada ya kuona shamba wanalolimiliki lenye ukubwa wa ekari nne (4) likiwa na migomba, nanasi pamoja na mihogo.

Bi. Martha Edward, Bi. Ester Constantine na Bi. Rhoda Nicodem ni baadhi ya walengwa wa mpango huu kutoka Nyambaya nao wameeleza kuwa, kupitia TASAF III wamewaweza kujenga nyumba wakiezeka kwa bati, kuwa na mifugo kama Kuku, Mbuzi na Ng’ombe, kununua mashamba na kukodi mashamba. Bi Martha kwa upande wake anamiliki nyumba mbili (2) za bati, mbuzi watatu (3), ng’ombe wawili (2) pamoja na kilimo cha biashara bila kusahau kusomesha watoto.

Kwa hakika shuhuda zilizotolewa na kuonekana, zimedhihirisha kazi kubwa inayofanywa na TASAF, jambo linalowafanya viongozi wa Nyambaya akiwemo Bw. Musa Kisena (mtendaji wa kijiji cha Nyambaya) na wa Halmashauri akiwemo Bw. January Bikuba ambaye ni kaimu mkurugenzi mtendaji na waratibu wa TASAF ngazi ya wilaya na mkoa kuona ipo haja ya kuongeza jitihada ya mafunzo ili kuwainua zaidi kiuchumi walengwa hao.

Awali katika taarifa ya mtendaji wa kijiji ilionesha kuwa, mpango huo ulianza mwezi julai, 2015 na hadi hivi sasa ni awamu ya ishirini na mbili (22) kwa walengwa sabini na nne (74) kupokea fedha na wote wamejiunga kwenye bima ya afya, lakini vilevile kuwa na mfuko wa kukopeshana kwa riba ya asilimia kumi (10%) na kurejesha kila mwisho wa mwezi, ikiwa walianza na hisa za zaidi ya sh. laki moja ishirini na nne (TShs.124,000/=) na hivi sasa kuwa na jumla ya sh. milioni moja na laki sita (Tshs.1,600,000/=).

Kweli TASAF ni Maendeleo



Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2022 YATOKA January 29, 2023
  • KARIBU UPATE FOMU YA USHIRIKI KWENYE MAOENSHO YA TANO YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2022 September 11, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) PARTICIPATION FORM September 12, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) SPONSORSHIP PACKAGES September 11, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Shigela Asisitiza Mambo Matatu, Kiapo cha Ma DC Geita

    January 30, 2023
  • RC Shigela Asisitiza Mambo Matatu, Kiapo cha Ma DC Geita

    January 30, 2023
  • “Mgogoro wa Shambani Humalizwa Shambani”. Asema RC Shigela.

    December 29, 2022
  • RC Shigela Akabidhi Zawadi za Rais Samia

    October 16, 2022
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa