• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TANROADS na TARURA Wapongezwa Ujenzi wa Barabara-Geita

Posted on: January 26th, 2022

Ikiwa ni siku chache kuelekea Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa RCC, Wajumbe wa Bodi ya Barabara RRB Mkoa wa Geita wamezipongeza taasisi za Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS  Mkoa wa GEITA na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanzania TARURA Wilaya ya Geita kufuatia utekelezaji mzuri wa miradi ya ujenzi wa barabara wilayani Geita.

Pongezi hizo zimetolewa Januari 26, 2022 wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Geita walipotembelea miradi mitatu ya ujenzi wa barabara, mbili zikiwa za kiwango cha Changarawe na moja ikiwa ni ya kiwango cha Lami Nyepesi na kuipongeza halmashauri ya mji Geita wa ujenzi wa barabara ya lami kwa mapato ya ndani huku wakisisitiza uzingatiaji vipimo na viwango vya barabara ili kupata thamani ya miradi.

Kiongozi wa msafara wa wajumbe hao ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mbogwe Mhe.Charles Kabeho amesema, wilaya ya Geita kwa ujumla imetekeleza vyema ujenzi wa barabara lakini pia ameishukuru serikali chini ya Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi kwani kwa ujenzi wa barabara hizo wananchi wataweza kufanya biashara wakisafirisha mazao yao lakini pia uwepo wa barabara hizo nzuri utasaidia shughuli za usafirishaji.

“kwanza tunaishukuru serikali kupitia Mhe.Rais kwa fedha zinazojenga barabara, vilevile tuwapongeze TANROADS na TARURA kwa barabara nzuri lakini pia TARURA niwaombe muhakikishe mkandarasi wa barabara ya Nyamikoma-Lwenge-Bugalama anafika mapema eneo la kazi kwaajili ya kumalizia kazi ndogo zilizobaki ikiwemo uwekaji alama kwenye daraja” alisema Mhe.Kabeho.

Wajumbe wengine walisisitiza juu ya halmashauri kukumbuka kujumuisha taa za barabarani kwenye mikataba ya ujenzi wa barabara za lami ili kuepuka kuchelewa kufunga taa za barabarani pamoja na uwekaji njia za waenda kwa miguu.

Kwa upande mwingine, wawakilishi wa taasisi za TANROADS na TARURA wamesema wataendelea kuzingatia ushauri uliotolewa na wajumbe hao ikiwemo ule wa kuboresha matengenezo kwenye barabara ya Nyankumbu-Nyang’hwale kupitia matengenezo maalum yaani Periodic Maintenance hata kabla ya lami kuanza kujengwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya usafiri na usafirishaji na kuepusha ajali na majanga mbalimbali yatokanayo na ubovu wa barabara.

Mwisho, wajumbe waliilekeza TANROADS Geita kufanya mawasiliano ya haraka na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA juu ya muafaka ni Gati lipi litatumika eneo la Nkome ili lami ya km20 itakayoanza kujengwa, ijengwe na kuelekezwa katika eneo sahihi kama mipango inavyoonesha.

Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Nyamikoma-Lwenge-Bugalama yenye urefu wa Km.23 kwa kiwango cha Changarawe, matengenezo ya muda maalum Periodic Maintanance barabara ya Geita-Nzera Junction-Nkome yenye urefu wa Km.58 kwa kiwango cha Changarawe na mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mwanza Junction-Jengo la Utawala GTC-Hospitali ya Mkoa-Nyumba za Askari (Siro Barracks)-Chuo cha VETA yenye urefu wa Km1.3  kwa kiwango cha lami nyepesi.



Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2022 YATOKA January 29, 2023
  • KARIBU UPATE FOMU YA USHIRIKI KWENYE MAOENSHO YA TANO YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2022 September 11, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) PARTICIPATION FORM September 12, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) SPONSORSHIP PACKAGES September 11, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Shigela Asisitiza Mambo Matatu, Kiapo cha Ma DC Geita

    January 30, 2023
  • RC Shigela Asisitiza Mambo Matatu, Kiapo cha Ma DC Geita

    January 30, 2023
  • “Mgogoro wa Shambani Humalizwa Shambani”. Asema RC Shigela.

    December 29, 2022
  • RC Shigela Akabidhi Zawadi za Rais Samia

    October 16, 2022
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa