• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TANAPA yafadhili ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, samani, Ofisi na Boti ya Doria Chato

Posted on: February 8th, 2018

TANAPA yafadhili ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, Ofisi na Boti ya Doria Wilayani Chato

Shirika la hifadhi ya Taifa (TANAPA) limedhadhili Wilaya Chato ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu wa shule mpya ya sekondari ya Kikumbaitale iliyopo kata ya Kigongo pamoja na Boti yenye injini kwa kijiji cha Mwekani vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 99.

Akikabidhi miradi hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Geita mwenyekiti ya Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata  ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale.

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA)  Dkt. Allan Kijazi amesema mradi  wa vyumba vya madarasa umetekelezwa kwa ushirikiano  wa TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe, kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni 6.

Aidha Dkt. Kijazi amesema TANAPA imeamua kufadhili boti ya kisasa yenye injini na maboya yenye thamani ya shilingimilioni 47 kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani  (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutoka na ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria “ nikutokana na ushirikiano huo TANAPA kupitia hifadhi ya kisiwa cha Rubondo ili pokea na kupitisha maombi toka kwa wananchi wa kijiji cha Mwelani na kuwapatia mradi wa Boti, injini na maboya yake ambayo itatumika kufanya doria katika ziwa Viktoria.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel ameishukuru TANAPA kwa ufadhili wa miradi hiyo na kuahidi kuwa mkoa utasimamia vyema miradi hiyo. AidhaMkuu wa mkoa wa Geita amewataka wakazi wa Chato kuendelea kutoa taarifa za kuhusia uvuvi haramu. Ameagiza wananchi wote kwa kushirikiana na viongozi kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ili kubaini nyavu haramu ambazo bado hazijasalimishwa.

Bodi ya wadhamini ya TANAPA ipo mkoani Geita kwa ajili ya vikao vya bodi hiyo ambavyo vinafanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo. Wakiwa Wilayani Chato wajumbe wa bodi ya wadhamini ya TANAPA walipatafursa ya kutembelea uwanja wa ndege wa Chato ambapo wamesema kukamilika kwa uwanja huo utasaidia kuibua fursa nyingi za kiuchumi na kuongezeka kwa idadi ya watalii kufika hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na hifadhi zingine zilizo jirani hasa katika mkoa wa Kigoma.

Matangazo

  • MATOEKEO YA KIDATO CHA SITA YATANGAZWA July 05, 2022
  • HOTUBA YA BAJETI YA NCHI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 June 01, 2022
  • BAJETI YA MKOA June 28, 2022
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Staki Senyamule Tarehe 19 Mei 2021 May 19, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • “Watumishi Jipangeni Kuwahudumia Wananchi, Ofisi Tunayo”- Asema RC Shigela

    August 06, 2022
  • “Sensa ni Kipaumbele Chetu Hadi Agosti 23, 2022”. Asema RC Shigella.

    August 05, 2022
  • “Sensa ni Kipaumbele Chetu Hadi Agosti 23, 2022”. Asema RC Shigella.

    August 05, 2022
  • Sensa si Mzaha, ni Maisha ya Watu, Tujiandae Kuhesabiwa-Asema RC Senyamule

    July 28, 2022
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa