• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC Shigela Asisitiza Mambo Matatu, Kiapo cha Ma DC Geita

Posted on: January 30th, 2023

Mkuu wa Mkoa Geita Mhe.Martine Shigela amesisitiza juu ya utendaji kazi na watu kuepuka kugeuza dhamana kuwa mali ya familia bali kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika utekelezaji wa majukumu ya serikali.

Mhe.Shigela amesema hayo Januari 30, 2023 wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya wapya watatu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Januari 25, 2023 ambapo watatu kati ya wanne ndiyo waliyokula kiapo.

“kwanza tumshukuru Rais Samia kwakuwa anaipenda Geita hata kuiletea watoto wenu, tena wa kutoka Geita. Hivyo muwape ushirikiano, msigeuze dhamana kuwa mali ya familia. Tuwape nafasi wafanye kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu”. Alisema RC Shigela.


Katika kuhitimisha, RC Shigela aliongeza kusema yapo mambo muhimu matatu ambayo viongozi hao wanapaswa kuzingatia akisema, “jukumu la wakuu wa wilaya linahusisha uongozi, yani ifahamike kuwa, kila kitu kinamhusu mtawala. Huwezi kutawala usilolijua, hivyo nendeni mkafanye mikutano, wasikilizeni wananchi. Na juu ya usimamizi, mambo yote yanapaswa kufanyika kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni na mwisho ni juu ya usalama, unahusu raia, mali, eneo na maisha ya watu, hivyo tatueni migogoro”

Nao kwa nyakati tofauti, Mhe.Said Nkumba DC Bukombe anayeendelea na kituo chake, Mhe.Grace Kingalame DC Nyang’hwale, Mhe. Deusdedith Katwale DC Chato na Mhe.Cornel Magembe DC Geita wamesema wanamshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia kwa kuwaamini na kuwateuwa kuwa wakuu wa wilaya na kuomba ushirikiano kwa wananchi, watendaji huku wakiomba viongozi wa dini kuwakumbuka katika maombi.

Kwa upande mwingine, mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Mhe.Nicholaus Kasendamila amewaombea viongozi hao kuwa na afya njema, hekima na busara katika kutekeleza majukumu yao akiwakumbusha kuwapenda wananchi, kuwasikiliza kisha akawakaribisha mkoani Geita.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, viongozi wa dini pamoja na taasisi binafsi.

Geita ya Samia, Hakuna Kilichosimama





Matangazo

  • WALIOCHAGULIWA MAFUNZO YA KILIMO KUPITIA PROGRAMU YA BBT-YIA FEBRUARI, 2023 March 16, 2023
  • KARIBU UPATE FOMU YA USHIRIKI KWENYE MAOENSHO YA TANO YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2022 September 11, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) PARTICIPATION FORM September 12, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) SPONSORSHIP PACKAGES September 11, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Zaidi ya Milioni 293 za RUWASA Zawatua Ndoo Kichwani Wananchi 10,448 Nzera&Bugando

    March 19, 2023
  • Tupeleke Mafunzo ya Mfumo wa PVMIS Ngazi za Vituo- Asema Dkt.Mkapa

    March 16, 2023
  • Mfumo wa PVMIS Kurahisisha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya-Geita

    March 14, 2023
  • Mfumo wa PVMIS Kurahisisha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya-Geita

    March 14, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa