• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC Gabriel Aagiza Kufanyika Uchunguzi Zahati ya Nyanguku Mjini Geita

Posted on: November 5th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, ameagiza kufanyika uchunguzi kufuatia nyufa/mipasuko iliyoonekana kwenye Zahanati ya Nyanguku iliyopo Kata ya Nyanguku Halmashauri ya Mji Geita.

Hayo yamejiri alipokuwa njiani kuelekea katika ziara yake ya kikazi kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo aliyoianza leo tarehe 05.11.2018 itakayofanyika mkoa mzima hivyo kupita katika Zahanati hiyo na kushangazwa na mipasuko iliyopo kwenye majengo hayo yanayokadiriwa kugharimu takribani Milioni Mia Mbili likiwa yamefunguliwa mapema mwezi januari mwaka 2018.

Kufuatia nyufa hizo, Mhandisi Gabriel ameagiza kushikiliwa kwa aliyekuwa Kaimu Mtendaji wa Kata ya Nyanguku Bw. Dionis Lubiyu ili asaidie kutoa maelezo ni kwa nini ujenzi haukuzingatia mahitaji yaliyopo kwenye makadirio ya gharama za ujenzi (BOQ), vilevile kuwatafuta wote waliosimamia mradi huo wakiwemo wataalamu ili kurudisha fedha ya serikali iliyopotea hadi kuwakosesha huduma wananchi.

Amesema, “yatupasa kuzingatia kanuni za ujenzi, tuwe wazalendo, ndipo tutaweza kuwatendea haki wananchi wetu kupitia miradi hii, TAKUKURU shughulikia suala hili, vilevile timu ya Mkurugenzi mara moja ianze uchunguzi na shughuli zisiendelee kwakuwa majengo haya ni hatari kutumiwa”

Kufuatia hali hiyo, tayari Mkoa umeandaa mfumo wa kusimamia na kuthibiti miradi yote inayotekelezwa ndani ya mkoa ambapo majaribio yatafanyika Halmashauri ya Mji na kwamba mfumo huo utakuwa na taarifa na picha za hatua mbalimbali kuanzia vifaa vya ujenzi, msingi, maboma n.k kuwa utakuwa ni mfumo utakaoweza kusaidia usimamiaji kuepuka changamoto kama ya Nyanguku.


Vilevile Mhandisi Gabriel ameagiza kutengwa kwa eneo jingine kwa ajii ya zahanati ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwa kwa sasa wananchi wanapata huduma za afya katika kituo cha afya Nyankumbu Mjini Geita huku akiagiza uchunguzi wa majengo yote ya elimu na afya ili kujiridhisha na ubora kuepuka madhara ya baadae, kisha kuendelea na ziara yake.



Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Waziri Mavunde Aaagiza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nyuma Ya CSR Geita

    April 15, 2025
  • Mabonanza ya Watumishi Yawe Endelevu - DC Kingalame

    March 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa