• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Nyang’hwale Yaibuka Kidedea Utoaji Bora wa Huduma za Afya

Posted on: July 28th, 2018

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amekabidhi Tuzo ya Ngao kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale  baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa kupata zaidi ya nyota tatu katika vituo vyake vyote vya kutolea huduma za afya Mkoani Geita. Ni katika ziara yake ya kikazi Mkoani Geita aliyoianza tarehe 26.07.2018.

Amesema “naipongeza Nyang’hwale kwa kupata asilimia tisini na tatu (93%) ya utoaji huduma bora za afya kwa maana ya kupata nyota kuanzia nyota tatu na kuendelea kwa kuwa pamoja na uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya afya ambayo serikali ya awamu ya tano imeufanya, sasa tunapima ubora wa huduma zinazotolewa”.

Amesema Geita ni mkoa wa tano katika ziara yake inayolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya afya ambapo lengo la serikali kwa sasa ni kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinapata kuanzia nyota tatu na kuendelea kwenye upande wa utoaji huduma bora za afya.

Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameeleza masikitiko yake kuhusu mimba za utotoni ambapo amesema wale wote watakaohusika kuanzia mzazi, mwalimu na wahusika wengine juu ya kuharibu maisha ya mtoto, wakamatwe na wawajibishwe kwa mujibu wa sheria. Pia ameshauri kamati ya Ulinzi na Usalama isaidiee kufanikisha suala hilo na ikiwezekana kesi za watoto zisizidi miezi miwili na kuwahimiza wazazi kutowafanya watoto kama mitaji yao kwa kupokea mahari na kuwaozesha lakini wengine wakiwatumikisha bila kusahahau kuanzisha kamati za ulinzi wa mama na mtoto kama njia moja wapo ya uzimamizi.

Amesema pia ni muhimu kwa serikali ya mkoa kutoa muongozo wa vipaumbele kwa taasisi zisizo za kiserikali zinazotarajia kufanya miradi yao kwenye mikoa husika kwani mkoa ndio unayajua mahitaji yake na pia walete taarifa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa ujio wake na kuhaidi kutekeleza maelekezo na kuongeza jitihada ili kufikia lengo la serikali kwa vituo vya kutolea huduma za afya mkoani kuwa na ubora wa kuanzia nyota tatu na kuendelea lakini pia amewapongeza Nyang’hwale kwa kujipatia tuzo hiyo na kuweka alama mkoani Geita hivyo wao ni chachu kwa mkoa na wengine waige waongezw bidii.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Joseph Odero ameeleza kuwa Hospitali ya Mkoa ina jumla ya watumishi 286 ambayo ni sawa na  42% na upungufu ni watumishi 395 ni sawa na 58% kulingana na ikama watumishi wanaohitajika katika Hospitali ya Mkoa ambao ni watumishi 681. Aliendelea kwa kutaja mafanikio yaliyopatikana yakiwepo kuimarika kwa hali ya Ubora wa utoaji wa huduma za afya vituoni kutokana na tathimni ya ubora wa huduma (health facilities star ranting) kutoka 42% mwaka 2015 ya vituo vyenye nyota hadi kufikia asilimia 98% mwaka 2017.

Matokeo ya Halmashauri za Mkoa wa Geita katika utoaji bora wa huduma za afya ni kama ifuatavyo;

1.    Nyang’hwale – 93%

2.    Mbogwe – 61%

3.    Chato – 43%

4.    Geita TC – 35%

5.    Geita DC – 17%

6.    Bukombe DC – 16%



Matangazo

  • WALIOCHAGULIWA MAFUNZO YA KILIMO KUPITIA PROGRAMU YA BBT-YIA FEBRUARI, 2023 March 16, 2023
  • KARIBU UPATE FOMU YA USHIRIKI KWENYE MAOENSHO YA TANO YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2022 September 11, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) PARTICIPATION FORM September 12, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) SPONSORSHIP PACKAGES September 11, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Zaidi ya Milioni 293 za RUWASA Zawatua Ndoo Kichwani Wananchi 10,448 Nzera&Bugando

    March 19, 2023
  • Tupeleke Mafunzo ya Mfumo wa PVMIS Ngazi za Vituo- Asema Dkt.Mkapa

    March 16, 2023
  • Mfumo wa PVMIS Kurahisisha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya-Geita

    March 14, 2023
  • Mfumo wa PVMIS Kurahisisha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya-Geita

    March 14, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa