• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA MKOA AZINDUA NA KUWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI SABA (7) HALMASHAURI YA MJI GEITA - MKOA WA GEITA

Posted on: May 13th, 2017

MKUU WA MKOA WA GEITA AZINDUA NA KUWEKA MAWE YA MSINGI KWENYE MIRADI SABA (7) YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MJI GEITA 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amefanya ziara  Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo amezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi Saba (7) ya Maendeleo.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amezindua vituo vitatu vya afya ambavyo ni kituo cha afya Mtakuja kilicho katika kata ya Mtakuja, Kituo cha afya Nyanguku kilichopokata ya Nyanguku na Kituo cha afya Shiloleli kilicho kata ya Shiloleli.  Aidha, ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa shule mpya Tumaini shule msingi iliyopo Nyankumbu mjini Geita, Ujenzi wa madarasa manne na ofisi ya kidato cha tano, Ujenzi wa Mabweni ya wasichana na Bwalo la chakula Shule ya Sekondari Kasamwa.

Mkuu wa Mkoa amepongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri hiyo na kuwataka kuendeleza jitihada hizo katika maeneo mengine ya Halmashauri ili wananchi wapate huduma katika mazingira mazuri na kuwataka wananchi kushirikiana na Serikali yao bega kwa bega ili kuongeza kasi ya maendeleo.

Awali akielezea miradi hiyo Mhandisi Modest Aporinali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita  amesema  kwamba Halmashauri hiyo imetenga  bajeti  ya shilingi milioni mia moja  na fedha hiyo ipo kwa kila mradi. Halmashauri ya Mji Geita ina mahitaji ya vituo kumi vya afya kwa sasa ina vituo viwili tu ambayo vinafanya kazi.Hata hivyo amesema Halmashauri hiyo inaendelea na jitihada za kutatua changamoto hiyo kwa kutumia mapato ya ndani na pia kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kama kampuni ya GGML ambayo imeahidi kiasi cha Shilingi milioni  mia moja kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mgusu.

Nao wananchi wamepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kwa kusaidia kusogeza huduma karibu na maeneo yao kwa kuwa zamani walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Na. (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita)

Matangazo

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Staki Senyamule Tarehe 19 Mei 2021 May 19, 2021
  • Vigezo vya Udhamini, Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji Kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita August 06, 2019
  • Matokeo Darasa la Nne Mkoa wa Geita January 11, 2018
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA -2018, MKOA WA GEITA December 11, 2017
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • “Maji Hayana Mbadala, Tutunze Chanzo cha Mto Nikonga”. Asema RC Geita

    June 26, 2022
  • Kuelekea Wiki ya Samia, RC Geita Akabidhi Pikipiki kwa Maafisa Ushirika

    June 24, 2022
  • Kuelekea Wiki ya Samia, RC Geita Akabidhi Pikipiki kwa Maafisa Ushirika

    June 24, 2022
  • Kuelekea Wiki ya Samia, RC Geita Akabidhi Pikipiki kwa Maafisa Ushirika

    June 24, 2022
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa