• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita yatoa Tamko la kumpongeza Rais Samia

Posted on: January 19th, 2022

Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Geita kwa kauli moja imetoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Utendaji uliotukuka wa kuliletea Taifa maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati iliyolenga kusogeza huduma za jamii kwa wananchi.

Halmashauri kuu ya CCM  imetoa tamko hilo leo januari 19, 2022 kwenye Ukumbi wa Nyerere-EPZA Mjini Geita wakati kamati hiyo ilipoketi mahsusi kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2021 kwa Mkoa huo.

Tamko hilo limekuja baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Mhe. Said Kalidushi kufafanua kuwa Mhe. Rais ameleta fedha nyingi kwenye Miradi mbalimbali Mkoani Geita na kuwa Mkoa wa tatu kwa kupata pesa nyingi zaidi nchini ambapo ndani ya kipindi cha serikali ya awamu ya sita kwenye miradi ya sekta mbalimbali, Mhe. Rais ameleta zaidi ya Tshs. Bilioni 58

"Kazi tumeiona, tumeona jinsi mlivyosimamia fedha za UVIKO na madarasa yanameremeta, sasa tunaomba shughuli zinazofanywa kwa nguvu za wananchi nazo mkazisimamie kama mlivyosimamia pesa hizi." Amesema ndg. Evarist Gervas MNEC Mkoa.

Kamisaa wa CCM Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Kamati yake kwa ufuatiliaji wa kina wa matumizi ya fedha za miradi na Wakuu wa Wilaya ambao wamesimamia kwa karibu miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora.

"Kwa kipindi cha kuanzia januari hadi desemba 2021 tumepokea zaidi ya Bilioni 58 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ukiachia mbali ile miradi ya kimkakati, fedha hizi ni nyingi sana na zimeletwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji, TASAF, Nishati ya Umeme na Barabaraba." Amesema



Matangazo

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Staki Senyamule Tarehe 19 Mei 2021 May 19, 2021
  • Vigezo vya Udhamini, Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji Kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita August 06, 2019
  • Matokeo Darasa la Nne Mkoa wa Geita January 11, 2018
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA -2018, MKOA WA GEITA December 11, 2017
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • “Serikali ni Mwajiri Bora Zaidi Tanzania”. Asema RC Geita Mhe.Rosemary Senyamule

    May 21, 2022
  • “Serikali ni Mwajiri Bora Zaidi Tanzania”. Asema RC Geita Mhe.Rosemary Senyamule

    May 21, 2022
  • “Serikali ni Mwajiri Bora Zaidi Tanzania”. Asema RC Geita Mhe.Rosemary Senyamule

    May 21, 2022
  • “Wananchi Tutumie Fursa ya Mzigo Flexi ya CRDB”. Asema RC Senyamule

    May 20, 2022
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa