Na Boaz Mazigo - Geita
Ni siku ya mwisho Septemba 4, 2022 kwa zoezi la kitaifa la utoaji Chanjo ya Polio awamu ya tatu tangu kuanza kwake Septemba Mosi, 2022 ambapo mkoa wa Geita umefanikiwa kuvuka lengo la kuchanja zaidi ya watoto 800,000 ambayo ni mafanikio kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla katika kufanikisha azma ya serikali kumlinda mtoto dhidi ya magonjwa mbalimbali ukiwemo huu wa Polio, ambao kama usipodhibitiwa unaweza kusababisha kupooza na pengine kifo kwa mtoto mwenye tatizo la upumuaji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mganga mkuu mkoa wa Geita Dkt.Japhet Simeo, mkoa wa Geita umechanja jumla ya watoto 890,907 kati ya lengo la watoto 728,158 sawa na asilimia 122.58. Hii ni hatua nzuri na ni kutokana na uratibu na usimamizi mzuri wa timu ya Chanjo Mkoa kwa kushirikiana na viongozi wa Kamati ya Usalama Mkoa hadi viongozi wa ngazi ya jamii (Mitaa, Vijiji na Vitongoji ) bila kusahau viongozi wa dini n.k.
Ikumbukwe kuwa, Septemba Mosi, mkuu wa mkoa Geita Mhe.Martine Shigela aliongoza kikao cha kamati ya msingi ya afya ngazi ya jamii (PHC) ambapo alihimiza kuwa, hakuna haja ya lengo kutokufikiwa ikiwa serikali chini ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan imewezesha upatikaji wa chanjo za kutosheleza mahitaji na hata kuzidi na kutoa wito kwa wananchi kuwapeleka watoto kupata chanjo ya polio kwani ni salama, haina madhara ila ni kwa ajili ya kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kupooza pamoja na kifo.
Kwa mkoa wa Geita, halmashauri ya wilaya Nyang’hwale imeongoza kwa kuchanja watoto 89,197 sawa na 137.15% ya lengo la watoto 65,038 ikifuatiwa na halmashauri ya wilaya ya Chato iliyochanja watoto 216,025 sawa na 130.13% ya lengo la watoto 166,776, halmashauri ya wilaya Mbogwe 97,118 sawa na 129.40 ya lengo, halmashauri ya mji Geita 100,613 sawa na 127.40, halmashauri ya wilaya Bukombe 107,897 sawa na 117.49% na halmashauri ya wilaya Geita kwa kuchanja watoto 280,057 sawa na 112.08 ya lengo.
Hii ndiyo Geita ya Dhahabu, Utajiri na Heshima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa