• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DKT. BITEKO AACHA ALAMA SEKTA YA MADINI

Posted on: September 23rd, 2023

EPZ Bombambili - Geita

Dondoo

-Tuzo imetolewa na Wachimbaji kutambua Mchango wake

- Madini Scheme Mbioni kuanza

- Sekta ya Madini imekua Sekta Kiongozi - Waziri Mavunde

- Mavunde atoa onyo kwa watoroshaji madini nchini

Imeelezwa kuwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ameacha alama kubwa katika Sekta ya Madini katika kipindi chote alichokuwa Waziri wa Madini na kupelekea mabadiliko makubwa katika sekta hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 23, 2023 na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Madini wakati Dkt. Biteko akifungua rasmi Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini katika viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita.

Akizungumza mara baada ya salaam hizo Dkt. Biteko amesema kuwa masuala yote yaliyozungumzwa na mafanikio hayo katika Sekta ya Madini yametokana usimamizi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sekta hiyo.

Kuhusu Waziri wa Madini Anthony Mavunde amemtaka afanye kazi kwa bidii na kuwataka wadau wa Sekta ya Madini nchini kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake kila siku.

"Vision 2030, Madini Maisha na Utajiri itachangia kuleta mabadiliko na kupunguza umaskini kwa wananchi wengi nchini, Sekta hii ni moyo wa uchumi wa nchi tuitumie kikamilifu ili kuleta mabadiliko," amesema Dkt. Biteko.

Aidha, ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kununua kilo 400 za dhahabu zilizosafiswa katika viwanda vya ndani vya kuchenjua dhahabu nchini. Ameitaka Benki Kuu kuwaunga mkono wachimbaji wa madini nchini ili kuleta tija na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini.

Kwa upande, wake Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa Dkt. Biteko ameifanya Sekta ya Madini imekua Sekta Kiongozi kwenye uchumi wa Nchi. Aidha ameipongeza mkoa wa Geita kwa kuandaa maonesho hayo kuwa yenye tija kwa wananchi wa mkoa wa Geita.

"Nimekuja na Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri ili hadi kufikia mwaka huo tuwe tumefanya tafiti katika eneo lote la nchi ya Tanzania ili wananchi wa waweze kunufaika na rasilimali madini," amesema Waziri Mavunde.

Pia, amesema ifikapo mwezi Oktoba Serikali itakabidhi mashine tano za uchorongaji wa Madini ili ziwe msaada kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema maonesho hayo yamefungua fursa za uwekezaji kwa wananchi wanaozunguka maeneo mbalimbali mkoani Geita kwa kubadilisha maisha ya jamii hiyo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Geita Constantine Kanyasu amesema kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Biteko ameacha alama kubwa katika Sekta ya Madini nchini. Aidha , ameongeza kuwa  mchango wake utakumbukwa katika nyanja zote hususan katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo na kuwawekea mazingira rafiki ya uchimbaji na uwekezaji.

Wengine walioshiriki katika ufunguzi huo ni Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Wabunge, Viongozi wa Vyama vya siasa,  Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Wakuu wa Taasisi za Umma na wadau mbalimbali wa sekta  ya madini.





Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Waziri Mavunde Aaagiza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nyuma Ya CSR Geita

    April 15, 2025
  • Mabonanza ya Watumishi Yawe Endelevu - DC Kingalame

    March 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa