• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Dkt. Avemaria Semakafu Azindua Usambazaji Nakala 3,583,750 za Vitabu vya Darasa la Tano

Posted on: December 23rd, 2018

Katika kufanikisha Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhusu kuboresha Elimu, zaidi ya shilingi za kitanzania Bilioni 6.8 zimetolewa na Serikali zilizowezesha uchapishaji wa nakala 3,583,750 zitakazosambazwa nchi nzima hadi kufikia mwezi Januari, 2019.

Akizundua zoezi hilo lililofanyika tarehe 22.12.2018 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu iliyopo Mjini Geita, Dkt. Avemaria Semakafu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwaniaba ya Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) Waziri mwenye dhamana na Elimu amesema, viongozi wanaosimamia elimu, wanao wajibu wa kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa asilimia zote lakini pia wahakikishe lengo la usambazi wa vitabu hivyo linafikiwa huku akiipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa jinsi walivyofanikisha utoaji wa vitabu mbambali ikiwemo vya darasa la pili, la tatu, la nne na vya la tano.

Amesema, “kwanza namshukuru Mhe.Rais kwa kutoa fedha za kufanyia shughuli hii, lakini pia niipotengeze TET kwa namna walivyofanya kazi hii kwa moyo na kuifanikisha na niwashukuru Geita kwa kunipokea”.

Dkt. Semakafu ameeleza kuwa, ni matarijio yake kuwa hadi kufikia Januari 7, 2019 vitabu vyote vitakuwa vimefika au kuwa katika hatua ya mbali ya usambazaji, huku akiwataka Maafisa Elimu na Wathibiti Ubora kwa pamoja wahakikishe vitabu vinafika mashuleni na vinapokelewa kwa mujibu wa taratibu za mapokezi, vinatumika na wanafunzi kwani vitabu kuwa vipya siyo sifa nzuri bali vyatakiwa kusomwa hata lengo lionekane kutimia.

Ameongeza kufafanua kuwa “vitabu hivi ni kwaajili ya darasa la tano mwaka 2019, hivyo walio madarasa ya mbele havitawahusu na kwamba huu ndiyo utaratibu wa kuondoa mtaala wa zamani.”

Amewataka wanafunzi kudai kupata vitabu ili wajisomee huku akisisitiza kuwa ni vyema vitabu hivyo ambavyo uwiano wake ni kitabu 1 kwa wanafunzi 3, viandikwe majina ya hao watakaovitumia na kwamba vinaposomwa vitabu hivyo, vitampa mwanafunzi uweo wa kuwa na ufahamu, udadisi, umakini na kumwezesha kupata maswali ya ziada kumuliza mwalimu. Na katika hili amewaambiwa walimu kuwa, wanapaswa kujiandaa kujibu ama kutoa ufafanuzi kwa wanafunzi, lakini  wao kama walimu wasikae na changamoto wanapokutana nazo bali waziwasilishe kwa waratibu elimu kata, maafisa elimu wilaya na wathibiti ubora, kwamba kwa namna hiyo watafanikiwa.

Ameupongeza uongozi wa serikali ya mkoa kupitia wawakilishi Bw. Denis Bandisa, Katibu Tawala Mkoa na Mwl. Shaban Kamchacho ambaye ni Afisa Elimu Mkoa kwa jitihada za kutatua changamoto ya uhaba wa miundombinu ya madarasa kwa kuwa na zaidi ya madarasa 8,000 yaliyo katika hatua mbalimbali za ujenzi, kisha kutangaza uzinduzi wa zoezi la usambazaji

Awali Dkt. Aneth Komba, Mkurugenzi Mkuu TET akisoma taarifa fupi ya kazi ya uandishi na usambazaji wa vitabu vya darasa la tano, amesema vitabu hivyo vinajumuisha masomo nane ambayo ni Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Stadi za Kazi, Maarifa ya Jamii, Sayansi na Teknolojia, Uraia na Maadili pamoja na Kifaransa na kwamba katika usambazaji wake, tayari zimeundwa kamati ya usambazaji hivyo ni tumaini la taasisi kwamba vitabu hivyo vitafika havitabaki maofisini kwa wakuu wa shule na kwenye halmashauri.

Akitoa neno fupi, Bw. Benjamin Oganga, Mkurugenzi Msaidizi, Elimu Sekondari kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewapongeza TET kwa namna ilivyofanikisha lakini pia kuwaasa viongozi kufuata maelekezo yote wakidumisha ushirikiano wanapotekeleza majukumu hayo.

Katika kuhitimisha, Prof. Benadetha Kilian na Mwenyekiti wa Bodi ya TET, alitoa neno la shukrani huku akiwahamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii ili nao waweze kufikia kiwango cha juu cha elimu wakilisaidia taifa.


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2022 YATOKA January 29, 2023
  • KARIBU UPATE FOMU YA USHIRIKI KWENYE MAOENSHO YA TANO YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2022 September 11, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) PARTICIPATION FORM September 12, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) SPONSORSHIP PACKAGES September 11, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Shigela Asisitiza Mambo Matatu, Kiapo cha Ma DC Geita

    January 30, 2023
  • RC Shigela Asisitiza Mambo Matatu, Kiapo cha Ma DC Geita

    January 30, 2023
  • “Mgogoro wa Shambani Humalizwa Shambani”. Asema RC Shigela.

    December 29, 2022
  • RC Shigela Akabidhi Zawadi za Rais Samia

    October 16, 2022
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa