Bilioni 9.2 Kutekeleza Miradi Mikubwa ya Viwanda, Elimu, Afya na Mazingira Mkoani Geita
Serikali Mkoani Geita imekusudia kuanzisha miradi mipya ikiwemo kiwanda cha sukari kutokana na mapato yanayotolewa na mgodi wa dhahabu wa GGM baada ya kuingia mkataba upya na halmashauri ya mji na wilaya ya Geita.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robart Gabriel wakati wa zoezi la kusaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya uchimbani wa madini ya dhahabu GGM wenye lengo la kuwanufaisha zaidi wananchi wa wilaya ya Geita na mkoa kwa ujumla. Amesema fedha zilizokwisha kutolewa na GGM kwa mwaka huu ni Bilioni tisa pointi mbili ( 9.2) ambapo fedha hizo zitatumika kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wawezesha wananchi kujikwamua na umasikini, kujenga kiwanda kikubwa cha sukari ,afya elimu na mazingira.
Ameongeza kuwa fedha hizo zitabadilisha mandhali ya Mji wa Geita pamoja na kuwezesha miradi ya elimu, afya na kuongeza kipato kwa Mkoa wa Geita baada ya kupata kiwanda.
Aidha, ameahidi kusimamia matumizi ya fedha na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaotumia fedha hizo kwa matumizi binafsi badala ya jamii na kujenga miundo mbinu ya kisasa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa