Seksheni hii ina lengo la kutoa huduma za kitaalamu zinazohitajika kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza Miundombinu na inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Miundombinu:
(i) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa sera za barabara, majengo,
nishati, maji taka, maji na mawasiliano.
(ii) Kusimamia ujenzi na ukarabati wa ofisi na majengo ya makazi
chini ya RS.
(iii) Kuwasiliana na mamlaka zinazohusika katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
kuhusu masuala ya uhandisi.
(iv) Kusimamia na kushauri juu ya kazi za uhandisi na miundombinu zinazofanywa katika
Mkoa
(v) Kutoa huduma za ukatibu kwa Bodi ya Barabara ya Mkoa.
(vi) Kufuatilia na Kutathmini Ujenzi wa Barabara, shughuli za ujenzi kwenye Halmashauri na TARURA.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa