• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Historia

Historia ya Mkoa wa Geita

Mkoa wa Geita ulianzishwa rasmi kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 02 Machi, 2012, na kuzinduliwa tarehe 08, Novemba, 2013 na Mheshimiwa DKT Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkoa huu ulitokana na sehemu ya Mikoa ya Mwanza, Kagera na Shinyanga ambapo upande wa Magharibi na Kusini unapakana na Mkoa wa Kagera, upande wa Kusini na Kusini Mashariki unapakana na Mkoa wa Shinyanga na Mwanza kwa upande wa Kaskazini unapakana na Ziwa Victoria.

Umbile la Mkoa na Maeneo ya Utawala

Mkoa huu una eneo au ukubwa wa kilometa za mraba 21,879 (Geita 6,375 km2, Bukombe 6,798 km2, Chato 3,572 km2, Mbogwe 3,684 km2, na Nyang`hwale 1,450 km2), kati ya hizo kilomita za mraba 19,933 niza nchi kavu na kilomita za mraba1,946 ni za maji.

Mkoa una Wilaya tano (5), Majimbo saba (7) ya Uchaguzi, Halmashauri sita (6), Mji mdogo 1, Tarafa23, Kata 122, Vijiji 474, Vitongoji 2,219 na Mitaa 65. Wilaya hizo ni Geita, Nyang‟hwale,Chato, Bukombe na Mbogwe.

Mkoa una jumuisha Halmashauri ya Mji Geita, Halmashauriza Wilaya za Geita, Nyang’hwale, Chato, Bukombe na Mbogwe. Kuanzishwa kwa Mkoa huu kumesaidia kuharakisha upelekaji wa huduma za kijamii, kiuchumi na maendeleo kwa wananchi.

Idadi ya Watu

Kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa una wakazi wapatao 2,977,608 ambapo wanaume ni 1,463,764 na wanawake ni 1,513,844

.

Idadi ya Watu Kiwilaya kwa Mwaka 2012

Wilaya
Jumla ya Wakazi
ME
KE
Wastani watu kwa Kaya 
Uwiano wa jinsia
Geita
807,619
400,475
407,144
5.9
98
Bukombe
224,542
110,857
113,685
5.9
98
Chato
365,127
181,365
183,759
6.0
99
Mbogwe
193,922
65,083
98,839
6.4
96
Nyang`hwale
148,320
73,272
75,048
6.8
98
Jumla
1,739,530
861,055
878,475
6.1
98

Chanzo: NBS, 2012

Hali yaHewa

Mkoa unapata mvua za kutosha kuanzia milimita 900 hadi 1200 na joto la wastani la nyuzi 22 hadi 30 kwa mwaka. Aidha, Mkoa umekuwa ukipata mvua za vuli katika kipindi cha kuanzia Septemba hadi Desemba na mvua za masika kuanzia mwishoni mwa mwezi Februari hadi Mei. Pia, kipindi cha kiangazi huanza mwanzoni mwa mwezi Juni hadi Septemba kila mwaka na unyevu wa kati ya asilimia 35 na 60.

Shughuli Za Kiuchumi na Pato la Mkoa

Wakazi wa Mkoa wa Geita wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji wa mifugo mbalimbali na nyuki, uvuvi, uchimbaji madini pamoja na biashara ndogo ndogo. Aidha, Sekta ya kilimo ina changia takribani asilimia 70 ya pato la Mkoa wa kati shughuli nyingine za kiuchumi zinachangia asilimia 30. Kwa mujibu wa takwimu kutoka NBS mwaka 2013 zinaonesha kuwa mchango wa Mkoa wa Geita katika pato la taifa umefikia shilingi bilioni 1,584 wakati Pato la mwananchi ni Shilingi 910,824.

Fursa za Uwekezaji zilizopo Mkoani Geita

Mkoa unafanya vizuri katika Uwekezaji na una zitangaza fursa mbali mbali zilizopo. Fursaza Uwekezaji katika Mkoa zipo katika Sekta za:- Kilimo, mifugo, madini, uvuvi, ujenzi, misitu na utalii. Pia hupatikana katika Sekta za Usafirishaji na Nishati. Mkoa unafanya jitihada mbalimbali za kuvutia wawekezaji na kuzinadi fursa za uwekezaji zilizopo ili wawekezaji waje kuwekeza na hatimaye kuongeza kasi ya maendeleo ya Mkoa. Baadhi ya wawekezaji ni Ukurwa Investments, Lake Gas, Lenny Hotel Limited, Waja Schools & Hospital, Makoye Hospital, Chobo Investiment, National Housing Cooperation, GGM na VETA.

Orodha ya Viongozi wa Mkoa wa Geita toka Kuanzishwa Kwake Mwaka 2012

1. Wakuu Wa Mikoa

NA.
JINA
CHEO
MWAKA
1.
Mhe. Magalula Said Magalula
Mkuu wa Mkoa
2012-2014
2.
Mhe. Fatma A. Mwassa
Mkuu wa Mkoa
2014-2016
3.
Mhe. Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga
Mkuu wa Mkoa
2016-2017
4.
Mhe. Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi
Mkuu wa Mkoa
2017-2020
5.
Mhe. Rosemary Staki Senyamule
Mkuu wa Mkoa
2020-2022
6
Mhe. Martine Shigela
Mkuu wa Mkoa
2022


2.Makatibu Tawala wa Mkoa

NA.
JINA
CHEO
MWAKA
1.
Ndugu. Severine Kahitwa
Katibu Tawala Mkoa
2012-2014
2.
Ndugu.Charles A. Pallangyo
Katibu Tawala Mkoa
2014- 2016
3.
Ndugu.Selestine M. Gesimba
Katibu Tawala Mkoa
2016-2018
4.
Ndugu. Denis I. Bandisa
Katibu Tawala Mkoa
2018-2020
5.
Ndugu. Mussa Chogero
Katibu Tawala Mkoa
2020-2022
6.
Prof.Godius Walter Kahyarara
Katibu Tawala Mkoa
2022-

Matangazo

  • WALIOCHAGULIWA MAFUNZO YA KILIMO KUPITIA PROGRAMU YA BBT-YIA FEBRUARI, 2023 March 16, 2023
  • KARIBU UPATE FOMU YA USHIRIKI KWENYE MAOENSHO YA TANO YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2022 September 11, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) PARTICIPATION FORM September 12, 2022
  • THE 5TH TANZANIA MINERALS TRADE FAIR (TMTF) SPONSORSHIP PACKAGES September 11, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Zaidi ya Milioni 293 za RUWASA Zawatua Ndoo Kichwani Wananchi 10,448 Nzera&Bugando

    March 19, 2023
  • Tupeleke Mafunzo ya Mfumo wa PVMIS Ngazi za Vituo- Asema Dkt.Mkapa

    March 16, 2023
  • Mfumo wa PVMIS Kurahisisha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya-Geita

    March 14, 2023
  • Mfumo wa PVMIS Kurahisisha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya-Geita

    March 14, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa