• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kero ya Umeme Kuwa Historia Geita. Ujenzi wa Kituo cha Kupozea Umeme Geita Eneo la Mpomvu Kuanza Wiki Ijayo.

Posted on: November 14th, 2018

Wataalam wa Kampuni ya China CAMC Engineering iliyopata zabuni kujenga kituo cha kupoozea umeme Geita eneo la mpomvu, tayari wamewasili  mkoani Geita tayari kwa kuanza ujenzi wa mradi huo baada ya zoezi la fidia lililokuwa likiendelea kukaribia tamati.

Akiongea kwa niaba ya wataalam alioambatana nao katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bw. Lane Lei amesema yeye na wenzake wamefurahi kufika Geita na wameyapenda mazingira huku akihaidi kuifanya kazi hiyo kwa muda uliopangwa ili kutatua kero ya wana Geita iliyokuwapo kwa muda mrefu sasa ya kukatika kwa umeme .

Amesema, “ tumefurahia kuwa Geita ni wakarimu na ni mahala salama, tumependa mchele wa huku ni mzuri na nafuu na tunakushukuru mkuu wa mkoa kwa kutupokea. Tutapenda na tupo tayari kufanya kazi ya jamii mkoani hapa kwani popote tunapofanya kazi ni lazima tuache kitu. Vilevile tutakuwa tayari kufanya kazi na wazawa wa Geita na Watanzania kwa kazi zilizopo kulingana na uhitaji”. alimaliza

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel akachukua fursa hiyo kuwahakikishia ulinzi na ushirikiano muda wote wawapo Geita lakini pia awaomba wasisite kujulisha kwa eneo lolote watakalokwama ili aweze kuwasaidia lengo ni kutekeleza mradi kwa wakati akiwaambia “nitafuteni masaa 24 nitakua tayari kuwasaidia”

Awali Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Medard Kalemani alimleta na kumtambulisha Mkandarasi huyo CAMC Engineering of China Mkoani Geita na kumuonesha eneo hilo tarehe 17.07.2018 ambapo lilifuata zoezi la fidia ili kuanza kwa ujenzi wa mradi huo na kwa kuwa ni mzoefu, Waziri Kalemani alisema anaamini atafanikisha utekelezaji wake tena kwa wakati, ufanisi na kasi inayozingatia ubora. Mhe. Waziri anaamini mradi huo utakamilika ifikapo Mei, 2019 kwa maana Mhe. Rais Magufuli tayari amewezesha mradi huo kwa kutoa Dola Milioni 123 za Kimarekani (123,000,000.USD) sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni Arobaini za Kitanzania.

Tukumbuke kuwa, serikali katika kutafuta suluhisho la kudumu la tatizo la umeme ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, inajenga Kituo kikubwa cha Kupozea umeme (Sub Station) ambacho kitaanza kujengwa wiki ijayo eneo la Mpomvu Mjini Geita, eneo lenye ukubwa wa takribani heka tano kitakachokuwa na uwezo wa 220/33KV, 2x50MVA ambazo ni takribani Megawati 96 yaani kitapokea Umeme wa Msongo wa Kilovolt 220 na kutoa Kilovolt 33 kisha kuvinufaisha vijiji kumi na moja (11) vitakavyopitiwa na mradi, na wakazi 1,424 walio jirani.  Mikoa jirani kama Mwanza na Kagera itaweza kunufaika umeme huu kwani ni wa kutosha.

Kati ya Megawati 96, Mgodi Mkubwa wa Dhahabu GGM utapewa Megawati 20, na zitakazobakia ni kwa wananchi. Kwa maana nyingine, wawekezaji endeleeni kuukaribia mkoa huu kwa kuwa mazingira rafiki ya kufanya biashara yanapatikana lakini Mgodi waa GGM waarifiwa kuendelea kujiandaa kupokea Megawati hizo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zao na kwa kufanya hivyo watakuwa wanafanya kazi kwa tija na kuchangia pato la taifa kwa kutumia umeme wa TANESCO.

Hiyvo basi, Serikali ya Mkoa inaendele kutoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais na Wizara ya Nishati kwa ujumla kwa kuhakikisha ahadi hii inatekelezwa, lakini pia wito unatolewa kwa wananchi kuitunza miundombinu hiyo wakati na baada ya kukamilika.




Matangazo

  • Taarifa ya Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA), 2018 Mkoa wa Geita January 04, 2019
  • Orodha ya Watumishi wa Umma wanaostahili kulipwa madeni ya mishahara February 08, 2018
  • Matokeo Darasa la Nne Mkoa wa Geita January 11, 2018
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA -2018, MKOA WA GEITA December 11, 2017
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wadau Wakutana Kutathimini Utekelezaji wa Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira

    February 14, 2019
  • “Ningependa Kuona Asilimia ya Maambukizi ya VVU Inafikia Sifuri (0) Tanzania”, Asema Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania.

    February 13, 2019
  • Geita na Kagera Wakutana Kuanza Utambuzi wa Mipaka ya Mikoa Kupunguza Migogoro ya Ardhi

    February 09, 2019
  • MDH Watambulishwa Rasmi Geita, Waja na Afya Kwanza

    February 07, 2019
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: Box 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: +255 653 006 604

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa